MJASILIAMALI ALIYE TOKA

INATOKA PART II
 
Anasema alifanya kazi hiyo kuanzia  mwaka 1990 mpaka 2003 na ndipo walipo hamia mkoani tabora, baada ya mumewake kupata uhamisho wa kikazi.

Anasimulia kuwa wakati akiwa mkoani tabora aliendelea na kazi yake ya kufundisha utengenezaji wa batiki, safari hii akiwafundisha hata waumini wa madehebu ya kiislamu pamoja na wapagani.

Alifungua duka kubwa la batiki na  nguo  aina zote kama vile suruari ,mashati, vitambaa vya suti, vitenge vya waksi, magauni ya akina mama, watoto nk ikiwa  ni utoaji huduma kwa jamii.

Alisema mwezi aprili mwaka 2009 wakati akiwa safarini mkoani mbeya kumuuguza mama mkwe wake , alipewa taarifa na wafanyakazi wake kwamba majambazi wamevunja duka na kuiba kila kitu.

Alisema kuwa pamoja na kupata  taarifa hizo lakini hakufadhaika sana kwa sababu alimtegemea sana mwenyezi mungu , kwamba atamrudishia zaidi ya vile vyote vilivyopotea.

Mwaka 2010 selina alijifunza utengenezaji wa sabuni za kuogea na kufulia za miche na za maji.


Alimtaja mwalimu wake kwa jina la elbariki mchau kuwa ndiye aliyemfundisha kutengeneza sabuni za aina mbalimbali , pamoja na somo la biashara la kujua faida na hasara.

Pia alimfundisha kutumia vitabu vya aina mbalimbali vya kupokelea na kutoa , na kumwelekeza  jinsi ya kusajili biashara.

Alisema kuwa anamshukuru sana mwalimu wake kwa  kumtoa katika janga la usingizi ,na kumfikisha hapa alipofikia leo.

Alisema alipo rudi nyumbani Mbeya mwaka 2011 alisikia tangazo redioni likiwahitaji wajasiliamali waende Sido wakachukue mafunzo ya kuendesha biashara zao kwa kutafuta masoko, kutunza kumbukumbu na kuendesha biashara kwa faida.

Kwa vile wajasiliamali wengi walijitokeza kwenye mafunzo hayo, ilibidi ufanye mchujo mkubwa ilikupata idadi ya watu wanaofikia 35.

Mafunzo yaliyokuwa yakitolewa yalikuwa ni ya miezi minne hivyo mchujo uliendelea kutolewa, kwa njia ya kufanya mitihani ambapo walio shindwa walikuwa wanaondolewa.

Selina alisema kuwa walewaliokuwa wanashinda kwenye hiyo mitihani ya kila mwenzi walikuwa wanapewa shilingi milioni 1.1 ya Ruzuku kwaajili ya kuinua biashara zao.

Akifafanua zaidi selina alisema kuwa yeye alipewa ruzuku ya shilingi milioni 4.4 kwa vile alikuwa miongoni mwa washindi wa miezi minne mfululizo.

Mpaka kufikia sasa mjasiliamali huyo anamiliki duka kubwa la sabuni za aina zote paoja na batiki lililopo katika maeneo ya uwanja wa maonyesho ya nanenane, mkabara na kituo cha polisi wa usalama barabarani na huku akiendelea na shuguli ya kuwafundisha wajasiliamali.

Selina amesema kuwa pamoja na kupitia matatizo mbalimbali kamavile kuibiwa kwenye duka lake na kumfilisi kabisa lakini malengo yake ya baadaye,ni kwamba iwapo atapata wafadhili anategemea kufungua shule yake ya ujasiliamali.

Mafunzo atakayo yatoa katika shule yake ni kama vile utengenezaji wa sabuni za miche, za kuogea, za maji aina zote, za chooni Multipurpose Detergent, Shower Jelly, shampoo, mishumaa, sabuni ya Ubuyu, Uyoga na Unga wa lishe.

Pia alizitaja batiki za aina zote na vikoi na ushonaji wa foronya, mashuka (kudalizi) pamoja na nguo aina mbalimbali, vipochi na vikapu.

Alisema pia kuwa watafundisha usindikaji wa vyakula mbalimbali mfano unga wa lishe, unga wa ubuyu, kusindika majani ya ubuyu, mafuta ya ubuyu, kusindika mboga mbalimbali za majani, Chilly Sauce, tomato Sauce, Mango Peacow Clips, Bisi na utengenezaji wa Keki za aina zote.

Mjasiliamali huyo pia alizitaja rangi za nyumba za maji na mafuta, na mwisho akasema atatoa mafunzo ya salon, na jinsi ya kuendesha biashara hiyo kwa faida.

Ametoa wito kwa wananchi kuto kukaa bule bila kufanya kazi hasahasa wakina mama, na badala yake wajishughulishe ili kuinua vipato vya familia zao na taifa kwa ujumla.

Na mwisho amewataka pia wazazi kuwaleta vijana wao pamoja na watu wazima kwenda kujifunza katika kampuni ya kiwanda cha sabuni cha mount Mbeya, ili wapate ujuzi kwa kujiendeshea maisha yao wenyewe.

Anapatikana kwa :0755 351381

Imeandaliwa na George Chanda, Mbeya
.