Elimtaa Tv: Wakulima wa viazi wanapoteza asilimia 10 ya pato wakati wa mavuno

WAKULIMA wa viazi Mikoa ya Iringa na Njombe wasanapoteza asilimia 60 ya mapato ya kwenye kilimo hicho kuanzia wakati wa palizi mpaka mavuno kutokana na uzembe na vitendea kazi duni vya kilimo hicho.
Wakizungumza na startv mkoani Njombe maafisa kilimo na wataalamu wa viazi wa mikoa ya Njombe na Iringa  wamesema kuwa uchafu wa mashamba na vifaa duni vinavyo tumika katika kilimo cha viazi vimekuwa vikipoteza mazao
Mtaalam wa uzalishaji wa mbegu anasema kuwa mbegu kitaalamu zimewekewa kiwango cha uzalishaji lakini wakulima wanakosea wakati wa palizi na kupoteza asilimia 40 na alilimia 10 huachwa shambani wakati wa mavuno.

Sagcot wanatafuta wadau wa kutoa elimu kwa maafisa kilimo 60 kutoka mikoa ya Njombe na Iringa kwa awamu nne ili kuwasaidia wakulima kuondoa upotevu huo mafunzo yanayo fadhiliwa na Delphy.


Kilimo cha viazi kwa mikoa ya Njombe na Iringa kimekuwa kililimwa kwa mazoea na wakulima kutumia mbegu za zamani kitu Kinacho wasababishia wakulima kuendelea kubaki maskini kutokana na mbegu hizo kutoa pato duni.