Zlatan Ibrahimovich aoneshwa mlango wa kutokea Manchester United.

Zilianza kama tetesi ambazo leo zimefikia tamati na kile kilichokuwa kikisemwa sana kuhusu Zlatan Ibrahimovich kimetimia kwani klabu ya Manchester United imemtosa rasmi Zlatan na sasa hataonekana katika msimu ujao wa ligi akiwa na mashetani hao wekundu.
Mkataba wa sasa wa Zlatan Ibrahimovich na klabu hiyo unaisha tarehe 30 mwezi huu na wengi walisema kutokana na majeruhi na kiasi kikubwa ambacho Ibrahimovich anapewa ilikuwa ni ngumu kwa United kumpa mkataba na ukizingatia kwamba tayari ana miaka 35.
Lakini pamoja na kutoongezewa mkataba mshambuliaji huyo toka nchini Sweden atabaki katika uangalizi wa madaktari wa Manchester United ili kutibu majeraha yanayomsumbua lakini dalili za kumuona Zlatan akiwa Old Trafford msimu ujao ni asilimia 0.
Toka anunuliwe toka PSG katika dirisha kubwa la usajili lililopita Zlatan Ibrahimovich amekuwa na msimu mzuri na klabu hiyo kwani alicheza michezo 41 akiwa na jezi ya Manchester na kufunga mabao 28 katika michezo yote aliyoitumikia klabu hiyo na akifanikiwa kubeba ngao ya hisani,Capital One na EUROPA.
Tayari klabu inayoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani ya Hertha Berlin wameonesha nia ya kumtaka Zlatan Ibrahimovich lakini tatizo kwao limekuwa fedha lakini wamekiri kumtamani Ibrahimovich na kumuomba afikirie kuhusu kushinda kombe la Bundesliga.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2s7qvcu
via IFTTT