Wakamatwa na dawa za kulevya Mwanza

Jeshi la Polisi Mwanza linawashikilia watu wanne baada ya kuwakuta na dawa za kulevya aina ya Mirungi mafungu 57 yenye ukubwa wa kilogramu 56.75 ambayo yalikuwa yamewekwa kwenye mabegi na magunia.
Kamanda wa Polisi Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa polisi waliwakamata watuhumiwa hao leo majira ya saa kumi na moja alfajiri katika mtaa wa Mbugani ‘A’ Kata ya Mbugani wilayani Nyamagana.
“Askari wakiwa kwenye doria na misako walifanikiwa kuwakamata watu wa nne waliofahamika kwa majina ya Thomas Zacharia (25), mkazi wa mtaa wa Unguja Mwanza, Ally Athumani (35) mkazi wa Kahama Shinyanga, Nyamurya Elia (35) mkazi wa mtaa wa Unguja Mwanza, na Stanslaus Mapinduzi Elias (41) mkazi wa Tarime, wakiwa na dawa za kulevya aina ya mirungi mafungu 57, yenye kiasi cha kilogramu 56.75, yakiwa yamemewekwa kwenye mabegi na magunia, kitendo ambacho ni kosa la jinai” ilisema taarifa ya Msangi
Kufuatia sakata hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wakazi wa jiji na mkoa wa Mwanza hususani vijana akiwataka kuacha kujihusisha na biashara za madawa kwani ni kosa kisheria.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sH604b
via IFTTT