UNAONAJE MPIRA UKIBADILISHWA NA SHERIA HIZI ZIKAPITISHWA?

The International Football Assosiation Board(TIFAB) ni asasi inayohusiana na masuala ya soka kimataifa, TIFAB imekaa na kuona kuna masuala ya sheria za soka yanabidi kujadiliwa na kama ikiwezekana zibadilishwe.
Kubwa ambalo limekuwa gumzo ni suala la kupunguza muda wa kucheza soka kutoka dakika 90 zinazotumika hivi sasa hadi kuwa dakika 60 ina maana kila kipindi kitakuwa ni cha dakika thelathini thelathini.
TIFAB wana hoja kuhusu hili kwani wanadai wachezaji wanapoteza sana muda wakiwa uwanjanj na hivyo ili kudhibiti suala hilo inabidi muda wa kucheza uwanjani ubanwe na kupunguza kuwa dakika 60.
Idea nyingine ya TIFAB ni mchezaji kujipasia/kujianzia wakati akipiga faulo au kona, sheria hii ni tofauti ya sasa ambapo ukianza mpira wa free kick au kona ni lazima umpasie mchezaji mwingine ndio mpira uendelee.
Sheria nyingine ya TIFAB wamependekeza kuwepo kwa saa ya uwanja ambayo yenyewe itakuwa inaanza pamoja na ya muamuzi na kumaliza pamoja na ile saa anayotumia muamuzi wa kati.
Pia TIFAB wametaka mpira wa free kick uwe unapigwa hata kama mpira unatembea(sio lazima kusimama) na penati ikipigwa kama kipa akipangua hairuhusiwi mchezaji mwingine kwenda kufunga.
Tayari sheria zilizopendekezwa na IFAB zimeanza kufanyiwa majaribio,ikiwemo ya kapteni tu kuongea na muamuzi ambayo imeanza kufanyiea majaribio katika michuano ya Confedaration Cup.
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sJxhq6
via IFTTT