Manchester Unites wasafishwa kesi ya Paul Pogba,Juve matatani

Lile sakata la kuhusu usajili wa Paul Pogba kwenda United bado halijaisha na upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea ambapo maofisa wa FIFA wanachunguza kila pande.
Suala la Pogba lilionekana kubwa pale ilipobainika kwamba wakala wa Pogba bwana Mino Raiola alipata karibia 50% ya pesa za usjili wa Pogba suala ambalo liliibua maswali kutokana na kiasi hicho cha pesa.
Sasa msemaji wa chama cha soka duniani FIFA ambao ndio wanachunguza suala hilo ametoa ufafanuzi kuhusu uchunguzi huo na kuwatoa Manchester United katika uchunguzi huo.
“Tumefungua mashtaka kuhusu Juventus kuhusiana na suala hilo na pia tumegundua upande wa Manchester United haukuwa na tatizo lolote katika usajili huo” alisema msemaji huyo.
Inaaminika kwamba Juventus walifanga ujanja ujanja na kuvunja sheria wakati wakimuuza Paul Pogba kwenda Manchester United na sasa watakuwa na kesi ya kujibu.

from Blogger http://ift.tt/2sP9zb2
via IFTTT