Kura ya Hapana yazua Mjadala Upitishaji Bajeti ya Serikali..Spika Ataka Waliopiga Hapana Wasipewe Pesa

Kauli ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kwamba waliopiga kura ya hapana wakati wa kupitisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 wasipatiwe fedha na mawaziri kwa ajili ya miradi imeibua mjadala bungeni.
Aliyeanza kuhoji kuhusu kauli hiyo leo (Jumanne) ni Joseph Mbilinyi maarufu Sugu aliyetaka mwongozo wa spika kuhusu kauli yake.
James Mbatia, amesema ni bora kufanyike mabadiliko ya Katiba ili kuwe na chama kimoja kama Bunge haliruhusu mawazo tofauti.
David Silinde amesema kauli zinazotolewa zinaweza kulipasua Taifa, hivyo kuwataka wabunge kutojenga Taifa ambalo wanaweza kulipasua wenyewe.
Mchungaji Peter Msigwa amesema wapinzani hawako bungeni kwa bahati mbaya na kwamba waliowachagua wanajua misimamo yao, hivyo wanapopiga kura ya hapana si kwamba Serikali ipeleke fedha kama hisani kwa kuwa ni fedha za walipa kodi.
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amesema dunia imebadilika na kwamba zamani bajeti haikuwa shirikishi lakini sasa wabunge wanashirikishwa tangu mipango na maoni ya pande zote huchukuliwa kwa hiyo inashangaza kukataa.
Spika amesema upinzani si wa kusema hapana kwa kila jambo hata pale unaposhiriki na kwamba, unaposema sitaki halafu ukamfuata waziri kwa ajili ya fedha za miradi ataangalia akusaidie vipi. Amesema hapo baadaye itabidi kuangalia namna ya kufany
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sPbKeV
via IFTTT