Blackberry yaishtaki Nokia kwa wizi wa teknolojia

Kampuni ya simu ya Blackberry inaishtaki Nokia kuhusu madai kwamba kampuni hiyo ya Finland imetumia uvumbuzi wake bila ruhusa.
Madai hayo ya ukiukaji yanahusisha teknolojia inayotumika katika 4G pamoja na mitandao mingine ya simu.
Kampuni hiyo ya Canada inadai kwamba transmita za Nokia pamoja na programu nyengime zinatumia teknolojia yake.
”Tunajua kwamba kuna malalamishi ,tutayajadili madai yaliotolewa na kuchukua hatua zinazohitajika kutetea haki zetu”,alisema msemaji
Kesi hiyo inasikizwa nchini Marekani.
Blackberry inataka kulipwa fedha badala ya kuizuia Nokia kutumia teknolojia yake kulingana na nakala za mahakamani zilizochapishwa na tovuti ya habari ya Ars Technica.
Madai hayo ni pamoja na yale yanayosema kwamba Nokia ilikuwa inajua uwepo wa uvumbuzi huo baada ya kujaribu kuununua hapo awali kabla ya Blackberry kuamua kutumia.
Kampuni hizo mbili zilizozana 2012 wakati Nokia ilipojaribu kuhakikisha kuwa mauzo ya simu za Blackberry yanapigwa marufuku nchini Marekani na Uingereza katika mzozo mwengine.
Kampuni zote mbili zimesitisha utengenezaji wa simu zao na badala yake wametoa leseni za haki ya umiliki wa simu zao kwa kwa watengenezaji wengine wa simu.

from Blogger http://ift.tt/2s3C0lo
via IFTTT