Wadau wa Ukimwi wakaa Njombe







WADAU  wa kupambana na maambukizi mapya ya Ukimwi mkoa w anjombe wamesema kuwa kunachangamoto ya baadhi ya watu kutoroka kupata dawa katika vituo vya kuchukulia dawa za kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi.

Imedaiwa kuwa baadh ya watu wamekuwa wakitoroka kutoka katika vituo vya kuchukulia dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi kwa kushawishiwa na baadhi ya viongozi wa dini kuwa watawaombia na waache kuchukua dawa hizo.

Wakizungumza katika mkutano wa wadau wa kupambana na virusi vya ukimwi mkoa w anjombe unaojumuisha viongozi wa dini wa dini zote na waratibu wa ukimwi mkoa na wilaya ya mkoa wa Njombe pamoja na wadau kutoka asasi mbalimbali za kupambana na maambukizo ya virusi vya ukimwi.

Mmoja wa wadau hao kutoka taasisi za kidini Elias Msemwa wa mkoani Njombe alisema kuwa kuna baadhi ya waumini wamekuwa wakikimbia dawa na kwenda kwa baadhi wa viongozi wa dini kuombewa ambapo baada ya kuacha dawa hizo asilimia kubwa ya hao hupotelea huko huko.

Alisema kuwa alifuatwa na muumini wake mmoja na kuambiwa kuwa anataka kwenda katika kituo kimoja cha maombezi ambacho kina waambia wasinywe dawa na watapona kitu ambacho hakukubaliana nachi na alimshauri muumini wake kuhusiana na tukio hilo na kuomba watumishe wenzake kuto washawishi watu kuachana na matumizi ya dawa.

Alisema kuwa baadhi ya watu wanao enda huko hupotelea huko humo baada ya kuacha dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi, na kusababisha watu hao kufa baada ya kuacha matumizi ya virusi vya Ukimwi.

Hata hivyo mratibu wa Ukimwi halmashauri ya Mji wa Njombe (Chac), Daniel Mwasongwe, alisema kuwa katika halmashauri yake kuna watu ambao wanakimbia katika vituo vya kuchukulia dawa na haijulikani kama wamefariki ama bado wapo wanaishi.

“Halmshauri ya Njombe kuna watu 7662 wanatumia dawa, 3496 wamehama,  14 wamepotea, wamepotea,  walio kimbia vituo vya kutolea dawa na wameacha kunywa dawa hii ni hatari kwa kuwa haijulikani kama watu hao wamekufa au wapo wanaishi,” alisema Mwasongwe.


Akiwasilisha tarifa ya halmashauri yake kuhusiana na mapambano ya Ukimwi na utekelezaji wa mapambano ya ugongwa huo alisema kuwa kuna watu, 18,460 Wanaoishi na virusi vya vya ukimwi halmashauri ya mji wa Njombe na waliandishishwa katika vituo vya huduma, 7662 wanatumia dawa, 14 wamepotea, 3496 wamehama  1433 wamekufa.