TFDA YATEKETEZA BIDHAA FEKI NJOMBE




MAMLAKA ya chakula na dawa nchini (TFDA) kanda ya nyanda za juu kusini imefanya msako wa bidhaa ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu mkoani njombe katika kaza za njombe Mjini na kata ya mtwango na kubaini bidhaa mbalimbali zenye thamani ya shilingi milioni 10.



Bidhaa hizo zimeteketezwa mkoani humo na mamlaka hiyo mbele ya kaimu mkuu wa mkoa wa njombe ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Ludewa Anatory Choya katika dampo la halmashauri ya mji wa Njombe Maheve.



Akizungumza wakati wa uteketezaji huo meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini Rodney Alananga aliema alisema uwa jamii imekuwa ikitumia bidhaa ambzo hazijasajiliwa kutumika hapa nchini, zilizo kushwa muda wa matumizi na zilizo pigwa marufuku kwa kuto kujua.



Alisema kuwa bidhaa walizo zikamata ni pamoja na zile ambazo hazona usajili wa kuuzwa hapa nchini, zilizo kusha muda wa matumizi hapa nchini na zile ambazo zimekuwa zikipigwa marufuku kama vipodozi na vinywaji vikali.



Alananga alizitaja badhi ya bidhaa ambazo wamezikamata ni pamoja na Soda, maziwa ya watoto aina ya Lactogen, vinywaji aina ya Dragon, Konyagi, rider pamoja na vitu mbalimbali ambavyo hutumika kama viungo.



“Kwa mfano bidhaa kama maziwa ya watoto wadogo aina ya Lactogen tumeyakuta hayajasajiliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), licha ya muda wake wa kutumika kuonyesha inamalizika mwakani, kiafya zinahatari kubwa kwa binadamu na watu wawe makini kuangalia muda wa kuisha matumizi” alisema Alananga na kuongeza.



“Tumefanya zoezi la siku mbili katika halmashauri ya mji wa Njombe pamoja na Kata ya Mtwango iliyopo katika wilaya ya Njombe na kufanikiwa kunasa bidhaa mbalimbali kwa wafanyabiashara 57 ambao wametoza faini ya kuteketeza vitu hivyo na wengine kufunga maduka yao,”




Akizungumza kabla ya kushiriki zoezi la kuteketeza bidhaa hizo kwa moto, Choya alisema serikali ya mkoa wa Njombe haitasita kuchukua hatua kali kwa wafanyabiashara wasio waaminifu kwa wateja wao.



“Kiama kinawajia, wajue kwamba serikali ina macho kama chandaluwa hivyo kwa kushirikiana na TFDA itawasaka wale wote wanaouza bidhaa zilizokwisha muda wake pamoja na bidhaa zisizo na ubora kwa binadamu, wito wangu kwa TFDA iendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwasaka wafanyabishara hawa wasio waaminifu,” alisema Choya.



Aliitaka TFDA kufungua ofisi katika mikoa mbalimbali nchini ili iweze kuendelea kutoa elimu kwa wananchi namna ya kutambua bidhaa feki zinavyoleta madhara kwa matumizi ya binadamu.



Hata hivyo Mratibu wa TFDA kutoka halmashauri ya mji Njombe, Inosensia Mtega alisema katika zoezi hilo wamebaini kuna wafanyabiashara mkoani Njombe wamekuwa wakiwauzia wananchi bidhaa zilizokwisha muda wake kwa bei ya jumla jambo ambalo ni hatari.



“Tumekuwa tukitoa elimu juu ya madhara ya vipodozi visivyotakiwa kwa matumizi ya mwanadamu, lakini bado kuna tatizo la elimu juu ya madhara hayo ya namna ya kubaini vipodozi visivyo


rasmi kwa matumizi ya binadamu,” alisema Mtega.