Wanawake wapeana somo la maadili


ZAIDI wanawake 850 wa jumuiya ya wanawake wa Kanisa la Uinjilisti Tanzania juzi wamekutana na kupeana somo la maadili mema ya kanisa kujenga na kujenga familia ya utii katika maisha ya Kikristo.
Jumuiya hiyo  iliyokusanya matawi 178 kati ya matawi 200 ya kanisa hilo, imekaa pamoja kwa kipindi cha siku tatu katika viwanja vya Ifisi vilivyopo katika Bonde la Songwe nje ya mji wa Mbalizi mkoani Mbeya, katika kipindi hicho walijifunza masomo matatu.
Mratibu wa mipango ya akina mama wa Kanisa hilo hapa Tanzania, Lydia Maag ameyataja masomo hayo kuwa ni Ndoa ya Kikristo, Uokovu na Ushuhuda wa wanawake wa Kikristo pamoja na somo 
Mratibu huyo amewapongeza viongozi wa Kanda kwa kuwahamasisha wanawake wenzao ili kufanikisha mkutano huo ambao ameutaja kama ni mkutano wa kihistoria uliohudhuriwa na wanawake kutoka mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa, Mpanda, Tabora na Shinyanga.
Lydia amesema jumuiya hiyo mwaka huu imefanikiwa kufanya mkusanyiko wa watu 850 wakati mwaka jana walikusanyika wanawake 650 na matokeo hao yanaonesha namna taifa lilivyo na wanawake wenye maadili mema.

Baadhi ya waumini wa jumuiya hiyo wamesema wamefundishwa mambo mengi ya kuwajenga kwenye familia zao ikiwa ni pamoja na kuwanyenyekea waume wao, kukabiliana na mbilnu za kukuza kipato cha kifamilia ili kuweza kupata fursa za kuwaendeleza vijana wao.
Naye Mkurugenzi wa mipango na maendeleo ya Kanisa Mchungaji Markus Lehner ameuipongeza jumuiya hiyo kwa jitihada zilizofanyika kwa kuwakusanya pamoja na lengo likiwa ni kupeana motisha na kuinua kanisa, kufarijiana katika Neno na katika Ukristo pamoja na kupeana taarifa za wanakotoka.
Mchungaji Lehner amesema ni baraka kubwa kwa kanisa ikizingatiwa kwamba sehemu kubwa ya kanisa inasimamiwa na akina mama ambao wamefanikiwa kuwakusanya wenzao kwa ghrama zitokanazo na vyanzo vya mapato ya idara ya wanawake wa kanisa hilo.