WATU 100 HUENDA 15 WAKAWA NA MAAMBUKIZI YA VVU

HALMASHAURI ya wilaya ya Njombe utafitu umebaini kuwa kila wanapo kutana watu 100 watu 15 wameambukizwa virusi vya ugonjwa wa ukimwi huku kila penye kundi la watu 100 watu 12 wamepima maambukizi ya virusi vya ukimwi hali ambayo inaashilia kuwa maambukizi yanazidi kuongezeka kila siku.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Njombe kwenye kikao cha kupambana na maambukizi ya virusi vya ukimwi kilicho wakutanisha viongozi wa halmashauri hiyo na viongozi wa madhehebu ya dini ili kutafta namna ya kuwanusuru wananchi na waumini na ugonjwa huo.

Dumba alisema kuwa katika halmashauri ya mji wa Njombe takwimu zinaonyesha kuwa maambukizi ya virusi yanakua kwa kasi katika  kundi la vijana na akina mama ambao wamekuwa wakibainika wakati wa kupimwa wakiwa na ujauzito.
Ametoa wito kwa wakina mama wajawazito kuendelea kujitokeza kupima ili kupata huduma ya kuwakinga watoto ambao hawajazaliwa kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa kuanza kutumia dawa za kinga.

Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Iluminata  Mwenda alinyesha kusiktishwa na hali ya maambukizi ya Ukimwi katika halmashauri ya hiyo na kueleza kuwa hilo pigo linalo sababisha maendeleo ya wakazi hao kudumaa  kutokana na vingozi na wadau wengine kutumia muda mwingi pamoja na rasilimali fedha kutafta namna ya kupambana na Ukimwi.

Hivyo aliwataka viongozi wa Dini kuhakikisha wanatoa elimu kwa waumini wao kwani watu wanao gundulika na maambu kizi wengi ao ni waumini na kuwa elimu ikitolewa kikamilifu wananchi wakatamua kuwa matumizi sahihi ya kinga na kujua namna ya kujikinga kwa kuwa na mpenzi mmoja ambapo wanahinizwa kuoa na kutulizana.

Kwa upandewa viongozi wa dini walio kuwepo katika mkutano huo waliiomba selikali kutoa elimu ya kutumia kinga vizuri na wao watafanya kazi ya kuweka hofu ya Mungu kwa waumini wao kutoka katika dini mbalimbali.

Mchungaji Bernard Sagaya alisema kwa upande wa serikali ifanyemajukumu yake ya kutoa elimu kwa wananchi na kuwa anawaomba viongozi wa serikali kujitokeza katika mikutano ya dini ili kukazia masomo yanayotolewa na viongozi hao katika mikutano yao mbalimbali na katika makanisa ili kufikia malengo ya kutokomeza Ukimwi

Mratibu wa Ukimwi halmashauri ya mji wa Njombe Daniel Mwasongwe alisema ameeleza changamoto zinazoyakabili mapambano dhidi ya Ukimwi na mikakati iliyopo kueneleza mapambano kuwa ni pamoja na kutokomeza maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto