Njombe yashuka kwa nafasi 2 matokeo ya darasa la saba





MKOA  wa Njombe umeshuka kwa na fasi mbili ya ufauru wa wanafunzi katika matokeo ya darasa la saba kutoka nafasi ya tano kitaifa na kushika nafasi ya saba na kushidhwa kufikia malengo ya matokeo makubwa sasa (BRN)kwa kufikisha alilimia 66 badala ya 79%.

Alisema kuwa licha ya kupanda kwa 6.5% bado mkoa huo haujafikia malengo ya BRN ya kitaifa kufikia alisima 79 na kuwataka maafisa elimu wa ngazi zote mkoani humo kuhakikisha wanafikia malengo kwa kusimamia maendeleo ya elimu.

Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Njombe Jackson Saitabahu alisema kuwa ni jukumu la kila afisa elimu wa kila halmashauri kuhakikisha elimu inasimamiwa kikamilifu ili kuleta maendeleo katika elimu na kuhakikisha kiwango cha kufauru kinaongezeka.

Aida alitoa maelekezi kwa kila halmashauri kufanya kikao cha tadhimini baada ya kikao hicho cha kupanga matokeo kwa kuhakikisha wanaangalia ni wapi wanakosea ili kuhakikisha katika matokeo ya mwaka ujao kiwango kinapanda na kufikia nafazi za juu klitaifa.

Alisema kuwa mkoa wa Njombe umewachukua watoto wote walio pata alama 100 hadi 250 wanafuzi ambapo ni wanafunzi  11,389, wanatarajiwa kuingioa kidato cha kwanza kwa mwaka huu na kuwa mkoa huo unajumla ya shule 480 na shule zilizo fanya mtihani ni shule 455.