WATU
wamekufa papo hapo katika ajali mbalimbali zilizo tokea Mkoani Mbeya ikiwemo ya
dereva bodaboda kugonga lori kwa nyumba na kufa papo hapo maeneo ya Mbalizi halmshauri
ya Mbeya Mkoani hapa.
Akizungumzia
ajali hizo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani alisema kuwa katika
ajali ya kwanza Dereva wa pikipiki maarufu Bodaboda, ambaye jina lake
halikufahamika alifariki dunia baada ya kugonga kwa lori.
Alsema
kuwa marehemu aliligonga lori lenyenamba za usajili namba T 388 BXS na Tela
namba T 183 ABX ambalo lilikuwa likiendeshwa na Joseph Kisinda ambapo pikipiki
hiyo ililigonga kwa nyuma.
Alisema
kuwa ajali hiyo ilitokea juzi majila ya saa 10:30 jioni katika maeneo ya Mbalizi
halmashauri ya Mbeya na mwili wa marehemu umehifadhiwa kati hospitali ya Ifisi
liliyopo halmashauri ya Mbeya.
Alisema
kuwa katika jajali ya pili gali aina ya Toyota Coster lenye namba za usajili T
561 BAJ likiendeshwa na Benard Mlimba lilimgonda Furaha Mwaipopo akiendesha
baiskeli mkazi wa Vwawa ambaye ni dereva wa bodaboda.
Alisema
kuwa marehemu alikuwa amempakiza mtu kwenye baiskeli na abilia wake Nione Sanga
alijeruhiwa katika ajali hiyo na anapatiwa matibabu kmatika Hospitali ya Vwawa wilayani
Mbozi.
Aliongeza
kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Vwawa na dereva wa gali
hiyo alitoloma mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Alisema
kuwa katika ajali ya tatu, Sailosi Cheyo aligonwa na Lori aina ya Fawn a kusababisha
kifo chake papo hapo wakati akijalibu kuvuka barabara.
Alisema
kuwa tukio hilo lilitokea katika maeneo ya kijiji cha Chimbuya Wilayani Mbozi
na gali hilo lenye namba za usajili T
509 BNP lenye tela namba T 231 BME likitokea Fingo Sijabaje mkazi wa Forest
Jijini Mbeya.
Alisema
kuwa ajali hiyo ilitokea mara baada ya galihiyo kuacha njia na kumvaa mtembea
kwa miguu huyo na kusababisha kifo chake.