WAJASILIAMALI WALIO KOPA KUPATA BIMA


WAFANYABIASHARA hapa nchini wataweza kupata bima ya mkopo kama atapata matatizo katika biashara yake anayoifanya kupitia mkopo.

Hayo yamebainishwa na Kaimu meneja taasisi ya Finca Mkoani Mbeya, Farida Hamisi muda mfupi baada ya kutabulisha akaunti mpya za taasisi hiyo kwa wadau wake.

Amesema kuwa wafanyabiashara waliokopa kutoka katika taasisi hiyo watanufaika na bima ya mkopo alikopa katika taasisi hiyo kama atapata matatizo katika biashara.

Alisema Taasisi hiyo sasa imepatiwa kibari kutoka katika benki kuu ya Tanzania cha kuwafungulia akaunti wateja wake ambao watanufaika na akauni hizo.

Alizitaja akaunti zinazo weza kufunguliwa katika taasisi hiyo kuwa ni poamoja na Akaunti ya Mkwanja na Malengo ambazo zitamuwezesha kupata liba kila mwezi.

Mfanyabiashara atapata bima kama atapata matatizo katika biashara yake iwapo kama atafiwa na mwenzake au kufariki yeye mwenyewe.

“Taasisi yetu ya Finca sasa wateja wetu watakao kopa watafunguliwa akaunti na kuweka marejesho yao katika taasisi yetu na sio kama ambapo mteja ilimlazimu kuweka katika taasisi zingime za kifedha” Alisema Hamis.

Alisema kuwa hivi karibuni taasisi hiyo inatarajia kuanzisha huduma za mikopo kwaajili ya wakulima na elimu ambazo zitazinduliwa mwisho wa mwaka huu.