RASIMU YA KATIBA: WAANDISHI WAJADIRI RASIMU
WAANDISHI wa habari mkoani Mbeya leo wanajadili rasimu ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na kuitaka katiba mpya kuwana serikali tatu huku wengine wakitaka serikali moja.
Asilimia kubwa ya katiba ya waandishi hao wanapendekeza kuwapo kwa Serikali moja ili kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali.
Waandishi habari wa walisema kuwa kumekuwa na serikali za mtaa ambapo serikali ambayo haitambuliki kikatiba naserikali hiyo inayo tambulika kikatiba.
Mmoja wa waandushi hao, Ally Kingo alisema kuwa katiba iwetambue Serikali ambayo yo itakuwa Tanganyika wakati nyingine Serikali ya Mapinduzi Zanzibar huku ikiwepo na ya muungano wa Tanzania.
Alisema kuwa wazanzibar wao tayari wanaserikali yao na katiba yao huku wakipeperusha bendera yao ambapo watanganyika serikali yao imekufa na kuwa ya muungano.
Kwa upande wake Moses Ng'wat alisema kuwa tuachane na mambo ya serikali tatu na kwani tushajichanganya na kuwapo kwa muungano huu kwani wazanzibar wameisha piga wimbo wao vya kutosha.
Kwani watanzania wanaingia Zanzibar kwa paspot na kukaguliwa huku wanaotoka Zanziba kuingia Tanzania bara wanaingia bila kukaguliwa.
Nae muwezeshaji wa majadiliano hayo, Mwangi Barnaba alisema kuwa kinacho pashwa ni kuwapo kwa serikali tatu na kwanini Tanzania na kuwataka waandishi hao kutaja nini kiondoke na nini kiingie katika Katiba hiyo.
mwisho