WANANCHI wakazi wa Mbalizi mkoani Mbeya wametoa maoni
mbalimbali katika Rasimu ya katiba iliyotangaza hivi karibuni wakitaka raisi
atangazwe baada ya kushinda kwa saidi ya asilimia 50.
Hayo yamebainishwa Juzi katika mkutano mapitio ya rasimu ya
katiba mpya ulioandaliwa na Asasi ya
Hope for Deprived Action in Deveropment (HDPAD), na kufanyika nje kidogo ya
mjimdogo wa Mbalizi na kuhusisha zaidi ya wakazi 80 na kutoa maoniyao.
Moja ya kundi la washiliki katika mkutano huo walipengekeza kuwa Rais
atatangazwa kuwa mshindi pale tu atakapo fanikiwa kufukisha kula zaidi ya
asilimia 50 ya kula zite zitakazo pigwa.
Kudi hilo likiongozwa na Eliud Mwambope alisema kuwa Mwambope
akizungumza kwa niaba ya kundi alisema kuwa kundi lake limependekeza kuwa raisi
atatangazwa kuwa ameshinda mpaka atakapo onekana amefikisha zaidi ya asilimia
50 ya kura zote za washiliki.
alisema kuwa ikitokea mgombea anaye ongoza hajafikisha
asilimia 50 inatakiwa uchaguzi uludiwe na Yule anaye mfuata ile sheria ya ‘simple
majority’ iondolewe.
“Tumependekeza kuwa Rais atatangazwa kuwa ni Mshindi baada ya
kushinda kwa zaidi ya asilimia 50 ikitokea hakuna aliyefikisha basi walio
fuatana katika uchaguzi huo warudie uchaguzi
ile sheria ya Simple majority iondolewe” Alisema
Pia katika uteuzi wa mawaziri Rais ateuwe mawaziri kulingana
na taaluma ya anaye teuliwa ili ufanisi katika utendaji kazi wa mawaziri.
Hivyo katika katiba mpya kuwepo na kipengele kinacho mrazimu
raisi kuteuwa mawazili walio na taaruma ya wizara husika.
Rasimu ya katiba mpya imeendelea kujadiliwa katika maeneo
mbalimbali hapa nchini kupitia mabaraza ya katiba waliyoandaliwa na taasisi
mbalimbali.