WAFANYABIASHARA hapa nchini wataweza kupata bima ya mkopo kama
atapata matatizo katika biashara yake anayoifanya kupitia mkopo.
Hayo yamebainishwa na Kaimu meneja taasisi ya Finca Mkoani
Mbeya, Farida Hamisi muda mfupi baada ya kutabulisha akaunti mpya za taasisi
hiyo kwa wadau wake.
Amesema kuwa wafanyabiashara waliokopa kutoka katika taasisi
hiyo watanufaika na bima ya mkopo alikopa katika taasisi hiyo kama atapata matatizo
katika biashara.
Alisema Taasisi hiyo sasa imepatiwa kibari kutoka katika
benki kuu ya Tanzania cha kuwafungulia akaunti wateja wake ambao watanufaika na
akauni hizo.
Alizitaja akaunti zinazo weza kufunguliwa katika taasisi hiyo
kuwa ni poamoja na Akaunti ya Mkwanja na Malengo ambazo zitamuwezesha kupata liba
kila mwezi.
Mfanyabiashara atapata bima kama atapata matatizo katika
biashara yake iwapo kama atafiwa na mwenzake au kufariki yeye mwenyewe.
“Taasisi yetu ya Finca sasa wateja wetu watakao kopa
watafunguliwa akaunti na kuweka marejesho yao katika taasisi yetu na sio kama
ambapo mteja ilimlazimu kuweka katika taasisi zingime za kifedha” Alisema
Hamis.
Alisema kuwa hivi karibuni taasisi hiyo inatarajia kuanzisha
huduma za mikopo kwaajili ya wakulima na elimu ambazo zitazinduliwa mwisho wa
mwaka huu.