TIMU ya Mbeya City imeitunishia misuli timu ya Ruvu Shoting kwa
kuichapa mabao 2-1 wakewa wenyeji wao mkoani Mbeya.
Meshihoyo ambayo imechezwa katika viwanja vya Sokoine jijini
Mbeya Mbeya City ikiwa mwenyeji wa Timu ya Ruvu Shoting, ilianza kwa kutikiza
nyavu za goli la mgeni wake katika dakika ya 8 katika kipindi cha kwanza
kupitia mchezaji wa timu hiyo John Kabanda.
KIKOASI CHA MBEYA CITY |
MBEYA CITY WAKISHANGILIA USHINDI WA GOLI LA PILI |
KOCHA WA TIMU YA MBEYA CITY JUMA MWAMBUSI |
Goli hilo la Mbeya city lilidumu kwa 13 kabla ya timu hiyo
kusawazisha katika dakika ya 25 ambapo ilitokea piga nikupige katika timu ya
Mbeya city na kumaliziwa na Paul Nonga.
Hadi dakika 45 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimetoshana
ubavu kwa kuwa na sale ya goli moja kwa moja.
MSEMAJI WA MBEYA CITY FREDY JACKSON a.k.a FREDOO |
CHARLES MKWASA KOCHA WA TIMU YA RUVU SHOTING |
Timu ya Mbeya City ambayo kwanza ndo inaingia katika
mtanange wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania haikulizika na sale wakiwa nyumbani
ambapo ilipo fika dakika ya 90 ya mchzo huo Stive Mazanda hakulizika na sale
hiyo na kisha kutikisa nyavu za mpinzani wake kwa kuutupia mpira golini.
Hadi mpira unamalizika timu ya Mbeya City imeibuka
kifuambele kwa ushindi wa bao 2-1 huku Ruvu Shoting waki ondoka kichwa chini.
Nae kocha wa Timu ya
Ruvu Shoting Charles Mkwasa alisema
kuwa ushindi wa Mbeya City ni waharali ila amemlalamikia muamuzi kwa kumaliza
mpira kabla ya Dakika 5 za nyongeza kumalizika mara baada ya timu yake kufungwa
goli la pili.
Kwa upande wake Juma Mwambusi Kocha wa Timu ya Mbeya City
amewataka mashabiki wa timu yake kuwa wavumilivu timu iwapo uwanjani.
Mwambusi amewataka mashabiki kuachana na lugha za matusi kwa
wachezaji na kuacha mpaka mpira umalizike kwani kwa kufanya hivyo wanawakatisha
tama wachezaji.
Timu ya Mbeya City huu ni ushindi wake wa Kwanza toka iingie
katika ligi hii ambapo katika ambapo katika mchezo wa kwanza walifurukuka kwa
kutoana jasho na timu ya Kagera sugar.
STORY PICHA NA HABARI ONLINE