MKANDA WABAKI BONGO, CHEKA AMSHINDA MMAREKANI PHILL WILLIAMS KWA POINT


Bondia Francis Cheka wa Tanzania (kulia) akimuadhibu mpinzani wake Mmarekani, Phill Williams, wakaati wa pambano lao la raundi 12 la kuwania Ubingwa wa Dunia uzito wa Super Middle (WBF) lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu. Katika pambano hilo Bondi Mtanzania Francis Cheka ameweza kumgalagaza kwa Pointi mpinzani wake na kutwaa ubingwa huo.
*******************
Na Mwandishi Wetu
HATA hivyo pambano hilo pamoja na yale ya utangulizi yaliingia dosari baada ya wachezaji kama Alfonce Mchumiatumbo, aliyekuwa akizichapa na Chupac Chipindi katika pambano lao la utangulizi la raundi sita, kugoma kupanda ulingoni kwa kile walichokuwa wakieleza mabondia hao kuwa wanahitaji kumaliziwa pesa zao za mkataba wa kucheza mechi hizo kabla ya kupanda ulingoni. 
Nao mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali, pia waligoma kupanda ulingoni wakishinikiza kumaliziwa pesa zao kwanza jambo ambalo lilifanya kuzua taflani ukumbini hapoa huku mapambano yakichelewa kuanza.
Ilipofika muda wa Cheka kupanda ulingoni pia alisikika mtangazaji akimuita muandaaji wa mapambano hayo ili kufika chumba alichokuwa Bondia mtanzania, Francis Cheka ili kumalizana naye mkwanja ili akubali kupanda ulingoni.
Alisikika Cheka akimuwakia muandaaji huyo kuwa, '' Nini Mmarekani hata angekuwa Mchina, nimalizie changu kwanza ili nipande ulingoni, ambalo pia lilichukua muda wa majadiliano hadi kuingiliwa kati na wadhamini na wadau wa ngumi waliotangaza kujikomiti kulipa pesa hizo wanazodai mabondia, ndipo mabondia hapo wakapanda ulingoni.

Aidha katika pambano la raundi 10 la mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali la kuwania Ubingwa wa WBF wa Afrika, Thomas Mashali ameweza kumshinda kwa pointi 2 tu mpinzani wake Mada Maugo na kutwaa Mkanda huo wa ubingwa wa WBF wa Afrika.
Na katika pambano la Utito wa Juu la utangulizi la Raundi sita kati ya Bondia Alfonce Mchumiatumbo na Chupac Chipindi, Mchumiatumbo amemchapa kwa KO mpinzani wake katika raundi ya tano, baada Chupac kunyoosha mikono juu kuashiria na wasaidizi wake kutupa taulo ulingoni kuashiria kushindwa kumalizia mchezo huo.  
 Waziri wa Habari, Fenella Mukangara (katikati) akipozi na mabondia Phill na Cheka, ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa pambano hilo la kimataifa.
 Waziri wa Habari, Fenella Mukangara (wa pili kushoto) akimvisha Mknda wa Ubingwa wa Dunia wa WBF Bondia Francis Cheka baada ya kumchapa kwa Pointi mpinzani wake Mmarekani, Phill Williams, katika pambano lao la raundi 12 lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu.
 Mashabiki wa Cheka wakifurahi na kumbeba baada ya kutangazwa mshindi.
 Bondia Mmarekani Phill Williams (kulia) akichapana na Francis Cheka wa Tanzania katika pambano lao lililomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
 Mabondia hao wakiliana Timing.......
 Cheka (kulia) na Phill wakichapana......
 Cheka (kulia) na Phill,wakiendelea kuchapana 
We subiri inakuja hiyooooo
 Sehemu ya mashabiki wa mchezo huo waliofurika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kumshuhudia Cheka akimchakza Mmarekani.
  Sehemu ya mashabiki wa mchezo huo waliofurika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kumshuhudia Cheka akimchakza Mmarekani.
 Baadhi ya wageni waalikwa walioshuhudia mchezo huo.
Bondia Mada Maugo (kulia) akimwadhibu mpinzani wake, Thomas 
Mashari kwa konde zito wakati wa pambano lao la raundi 10 la kuwania ubingwa wa Dunia wa WBF, ambapo Mashali ameibuka mshindi kwa 
Pointi dhidi ya Maugo. SOURCRE: Sufiani Mafoto Blog.

RAIS ATEUWE MAWAZIRI WALIO NA TAARIMA YA WIZARA HUSIKA


WANANCHI wakazi wa Mbalizi mkoani Mbeya wametoa maoni mbalimbali katika Rasimu ya katiba iliyotangaza hivi karibuni wakitaka raisi atangazwe baada ya kushinda kwa saidi ya asilimia 50.
 
Hayo yamebainishwa Juzi katika mkutano mapitio ya rasimu ya katiba mpya  ulioandaliwa na Asasi ya Hope for Deprived Action in Deveropment (HDPAD), na kufanyika nje kidogo ya mjimdogo wa Mbalizi na kuhusisha zaidi ya wakazi 80 na kutoa maoniyao.

Moja ya kundi la washiliki katika  mkutano huo walipengekeza kuwa Rais atatangazwa kuwa mshindi pale tu atakapo fanikiwa kufukisha kula zaidi ya asilimia 50 ya kula zite zitakazo pigwa.

Kudi hilo likiongozwa na Eliud Mwambope alisema kuwa Mwambope akizungumza kwa niaba ya kundi alisema kuwa kundi lake limependekeza kuwa raisi atatangazwa kuwa ameshinda mpaka atakapo onekana amefikisha zaidi ya asilimia 50 ya kura zote za washiliki.

alisema kuwa ikitokea mgombea anaye ongoza hajafikisha asilimia 50 inatakiwa uchaguzi uludiwe na Yule anaye mfuata ile sheria ya ‘simple majority’ iondolewe.

“Tumependekeza kuwa Rais atatangazwa kuwa ni Mshindi baada ya kushinda kwa zaidi ya asilimia 50 ikitokea hakuna aliyefikisha basi walio fuatana katika uchaguzi huo warudie uchaguzi  ile sheria ya Simple majority iondolewe” Alisema  

Pia katika uteuzi wa mawaziri Rais ateuwe mawaziri kulingana na taaluma ya anaye teuliwa ili ufanisi katika utendaji kazi wa mawaziri.
Hivyo katika katiba mpya kuwepo na kipengele kinacho mrazimu raisi kuteuwa mawazili walio na taaruma ya wizara husika.

Rasimu ya katiba mpya imeendelea kujadiliwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini kupitia mabaraza ya katiba waliyoandaliwa na taasisi mbalimbali.


MTOTO WA DARAZA LA PILI AFARIKI DUNIA
MTOTO Pasto Furaha (11) mwanafuzi wa daraza la pili, mkazi wa kijiji cha Mapinduka kata ya Igurusi wilayani Mbarali mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya kugongwa na lori.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Diwani Athumani alisema kuwa mtoto huyo aligongwa na roli hilo Juzi majira ya 12:30 jioni katika maeneo ya Mwapimbuka barabara ya Mbeya- Iruinga mkoani Mbeya.

Alisema Marehemu huyo alifariki wakati akipatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Igurusi na mwili wake umehifadhiwa kituoni hapo.

Alisema kuwa mtoto huyo alikuwa mwanafunzi wa daraza la Pili katika shule ya msingi Igurusi ya wilayani humo.

Athumani alisema kuwa gari hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Habibu Hassan (28) likiwa na namba za usajili T 877 CLX na trela namba T 242 CLV aina na Iveco.

Alisema kuwa gari hiyo inashikiliwa na Polisi na lipo katika kituo cha polisi cha kata ya Igurusi.

Aliongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwengo kasi wa dereva wa roli hilo la mizigo na akasababisha ajali hiyo.
Athumani alisema kuwa jeshi la Polisi linatoa wito kwa watumiaji wa barabara kuwa makini na madereva kuwajali watembea kwa miguu.MWANAPAZI "KATIBA HII SIO CHAMA WALA DINI"Haya ni matokeo kwa waliopiga kura ya kupendekeza muundo wa serikali tatu
KATIKA uchangiaji na kutoa maoni katika rasimu ya katiba Mpya wananchi wametakiwa kutoingiza itikadi za kisiasa wakati wa kuchangia.

Akifungua baraza la Katiba lililoandaliwa na Asasi ya Hope for Deprived Action in Deveropment (HDPAD) ya Mji mdogo wa Mbalizi jana Afisa Mtendaji wa Kata ya Usongwe, halmashauri ya Mbeya, John Mwanapazi alisema kuwa wajumbe katika katiba hilo wasionyeshe itikadi yoyote.

Alisema kuwa wanao changia katika baraza hilo wasipinge kile kilichopo katika Rasimu hiyo kwa kuonyesha itikadi ya aina yoyote iwe ya kidini ama kisiasa.

“Katiba hii ni ya Tanzania sio ya kanisa ama dini yeyote na sio katiba ya chama chochote cha kisiasa maoni yako yasiwe kamelenga katika chama Fulani au kanisa unalotokea,” Alisema Mwanapazi

Aliongeza Katiba hii siyo ya Chadema, CCM wala CUF katiba hii ni yawatanzania wote ya kizazi cha sasa na kijacho.

Alisema kuwa katika mapitio hao wasije wakaingiza chuki binafsi kwa kuwa watu wanaugomvi wao wakapingana  katika maoni yao.

Aliongeza kuwa katika maoni yao waangalie kuwa wanatoa maoni ambayo ni ya taifa na sio ya kwao binafsi na kulenga kila kona ya nchi yetu.

“Ndugu washiriki hakikisheni maoni unayo yatoa yawe yamelenga katika mrengo wa kitaifa zaidi na sio kuangalia kwa upanda wa kikata,” Alisema Mwanapazi

Hope for Deprived Action in Deveropment (HDPAD) WFANYA BARAZA RA KATIBAKATIKA KAYA YA USONGWE HALMASHAURI YA MBEYA

 Afisa Mtendaji wa kata ya Usongwe halmashauri ya Mbeya, John Mwanapazi akifungua baraza la Katiba katika kata yake lililo andaliwa na Asasi Hope for Deprived Action in Deveropment (HDPAD) 

Mmoja wa washiriki katika baraza ra katiba, Yohanes Mligo akitoa maoni yake katika Rasimu ya Katiba Mpya  katika mkunano wa kutoa maoni kuhusiana na Rasimu hiyo. (Ficha na Furaha Eliab, Mbeya)

Mmoja wa wajumbe wa wananchi wajio shiriki katika baraza ra katiba lililoandaliwa na Asasi Hope for Deprived Action in Deveropment (HDPAD), akifafanua jambo katika baraza hilo jana, (Picha na Furaha Eliab, Mbeya)

MBEYA CITY WAMLAZA RUVU SHOTING 2-1
TIMU ya Mbeya City imeitunishia misuli timu ya Ruvu Shoting kwa kuichapa mabao 2-1 wakewa wenyeji wao mkoani Mbeya.

Meshihoyo ambayo imechezwa katika viwanja vya Sokoine jijini Mbeya Mbeya City ikiwa mwenyeji wa Timu ya Ruvu Shoting, ilianza kwa kutikiza nyavu za goli la mgeni wake katika dakika ya 8 katika kipindi cha kwanza kupitia mchezaji wa timu hiyo John Kabanda.

KIKOASI CHA MBEYA CITY

MBEYA CITY WAKISHANGILIA USHINDI WA GOLI LA PILI

KOCHA WA TIMU YA MBEYA CITY JUMA MWAMBUSIGoli hilo la Mbeya city lilidumu kwa 13 kabla ya timu hiyo kusawazisha katika dakika ya 25 ambapo ilitokea piga nikupige katika timu ya Mbeya city na kumaliziwa na Paul Nonga.
Hadi dakika 45 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimetoshana ubavu kwa kuwa na sale ya goli moja kwa moja.
MSEMAJI WA MBEYA CITY FREDY JACKSON a.k.a FREDOO

CHARLES MKWASA KOCHA WA TIMU YA RUVU SHOTING
Timu ya Mbeya City ambayo kwanza ndo inaingia katika mtanange wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania haikulizika na sale wakiwa nyumbani ambapo ilipo fika dakika ya 90 ya mchzo huo Stive Mazanda hakulizika na sale hiyo na kisha kutikisa nyavu za mpinzani wake kwa kuutupia mpira golini.

Hadi mpira unamalizika timu ya Mbeya City imeibuka kifuambele kwa ushindi wa bao 2-1 huku Ruvu Shoting waki ondoka kichwa chini.

Nae kocha wa Timu ya  Ruvu Shoting Charles  Mkwasa alisema kuwa ushindi wa Mbeya City ni waharali ila amemlalamikia muamuzi kwa kumaliza mpira kabla ya Dakika 5 za nyongeza kumalizika mara baada ya timu yake kufungwa goli la pili.

Kwa upande wake Juma Mwambusi Kocha wa Timu ya Mbeya City amewataka mashabiki wa timu yake kuwa wavumilivu timu iwapo uwanjani.

Mwambusi amewataka mashabiki kuachana na lugha za matusi kwa wachezaji na kuacha mpaka mpira umalizike kwani kwa kufanya hivyo wanawakatisha tama wachezaji.

Timu ya Mbeya City huu ni ushindi wake wa Kwanza toka iingie katika ligi hii ambapo katika ambapo katika mchezo wa kwanza walifurukuka kwa kutoana jasho na timu ya Kagera sugar.

STORY PICHA NA  HABARI ONLINE 
  

WAJASILIAMALI WALIO KOPA KUPATA BIMA


WAFANYABIASHARA hapa nchini wataweza kupata bima ya mkopo kama atapata matatizo katika biashara yake anayoifanya kupitia mkopo.

Hayo yamebainishwa na Kaimu meneja taasisi ya Finca Mkoani Mbeya, Farida Hamisi muda mfupi baada ya kutabulisha akaunti mpya za taasisi hiyo kwa wadau wake.

Amesema kuwa wafanyabiashara waliokopa kutoka katika taasisi hiyo watanufaika na bima ya mkopo alikopa katika taasisi hiyo kama atapata matatizo katika biashara.

Alisema Taasisi hiyo sasa imepatiwa kibari kutoka katika benki kuu ya Tanzania cha kuwafungulia akaunti wateja wake ambao watanufaika na akauni hizo.

Alizitaja akaunti zinazo weza kufunguliwa katika taasisi hiyo kuwa ni poamoja na Akaunti ya Mkwanja na Malengo ambazo zitamuwezesha kupata liba kila mwezi.

Mfanyabiashara atapata bima kama atapata matatizo katika biashara yake iwapo kama atafiwa na mwenzake au kufariki yeye mwenyewe.

“Taasisi yetu ya Finca sasa wateja wetu watakao kopa watafunguliwa akaunti na kuweka marejesho yao katika taasisi yetu na sio kama ambapo mteja ilimlazimu kuweka katika taasisi zingime za kifedha” Alisema Hamis.

Alisema kuwa hivi karibuni taasisi hiyo inatarajia kuanzisha huduma za mikopo kwaajili ya wakulima na elimu ambazo zitazinduliwa mwisho wa mwaka huu.

RASIMU YA KATIBA: WAANDISHI WAJADIRI RASIMU


WAANDISHI wa habari mkoani Mbeya leo wanajadili rasimu ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na kuitaka katiba mpya kuwana serikali tatu huku wengine wakitaka serikali moja.

Asilimia kubwa ya katiba ya waandishi hao wanapendekeza kuwapo kwa Serikali moja ili kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali.

Waandishi habari wa walisema kuwa kumekuwa na serikali za mtaa ambapo serikali ambayo haitambuliki kikatiba naserikali hiyo inayo tambulika kikatiba.

Mmoja wa waandushi hao, Ally Kingo alisema kuwa katiba iwetambue Serikali ambayo yo itakuwa Tanganyika wakati nyingine Serikali ya Mapinduzi Zanzibar huku ikiwepo na ya muungano  wa Tanzania.

Alisema kuwa wazanzibar wao tayari wanaserikali yao na katiba yao huku wakipeperusha bendera yao ambapo watanganyika serikali yao imekufa na kuwa ya muungano.

Kwa upande wake Moses Ng'wat alisema kuwa tuachane na mambo ya serikali tatu na kwani tushajichanganya na kuwapo kwa muungano huu kwani wazanzibar wameisha piga wimbo wao vya kutosha.

Kwani watanzania wanaingia Zanzibar kwa paspot na kukaguliwa huku wanaotoka Zanziba kuingia Tanzania bara wanaingia bila kukaguliwa.

Nae muwezeshaji wa majadiliano hayo, Mwangi Barnaba alisema kuwa kinacho pashwa ni kuwapo kwa serikali tatu na kwanini Tanzania na kuwataka waandishi hao kutaja nini kiondoke na nini kiingie katika Katiba hiyo.

mwisho

NUNUENI MASHINE KUTOKA TANZANIA


WAFANYABIASHARA hapa nchini wataweza kupata bima ya mkopo kama atapata matatizo katika biashara yake anayoifanya kupitia mkopo.

Hayo yamebainishwa na Kaimu meneja taasisi ya Finca Mkoani Mbeya, Farida Hamisi muda mfupi baada ya kutabulisha akaunti mpya za taasisi hiyo kwa wadau wake.

Amesema kuwa wafanyabiashara waliokopa kutoka katika taasisi hiyo watanufaika na bima ya mkopo alikopa katika taasisi hiyo kama atapata matatizo katika biashara.

Alisema Taasisi hiyo sasa imepatiwa kibari kutoka katika benki kuu ya Tanzania cha kuwafungulia akaunti wateja wake ambao watanufaika na akauni hizo.

Alizitaja akaunti zinazo weza kufunguliwa katika taasisi hiyo kuwa ni poamoja na Akaunti ya Mkwanja na Malengo ambazo zitamuwezesha kupata liba kila mwezi.

Mfanyabiashara atapata bima kama atapata matatizo katika biashara yake iwapo kama atafiwa na mwenzake au kufariki yeye mwenyewe.

“Taasisi yetu ya Finca sasa wateja wetu watakao kopa watafunguliwa akaunti na kuweka marejesho yao katika taasisi yetu na sio kama ambapo mteja ilimlazimu kuweka katika taasisi zingime za kifedha” Alisema Hamis.

Alisema kuwa hivi karibuni taasisi hiyo inatarajia kuanzisha huduma za mikopo kwaajili ya wakulima na elimu ambazo zitazinduliwa mwisho wa mwaka huu.

WATATU WAFA KATIKA AJALI
WATU wamekufa papo hapo katika ajali mbalimbali zilizo tokea Mkoani Mbeya ikiwemo ya dereva bodaboda kugonga lori kwa nyumba na kufa papo hapo maeneo ya Mbalizi halmshauri ya Mbeya Mkoani hapa.

Akizungumzia ajali hizo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani alisema kuwa katika ajali ya kwanza Dereva wa pikipiki maarufu Bodaboda, ambaye jina lake halikufahamika alifariki dunia baada ya kugonga kwa lori.

Alsema kuwa marehemu aliligonga lori lenyenamba za usajili namba T 388 BXS na Tela namba T 183 ABX ambalo lilikuwa likiendeshwa na Joseph Kisinda ambapo pikipiki hiyo ililigonga kwa nyuma.

Alisema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi majila ya saa 10:30 jioni katika maeneo ya Mbalizi halmashauri ya Mbeya na mwili wa marehemu umehifadhiwa kati hospitali ya Ifisi liliyopo halmashauri ya Mbeya.

Alisema kuwa katika jajali ya pili gali aina ya Toyota Coster lenye namba za usajili T 561 BAJ likiendeshwa na Benard Mlimba lilimgonda Furaha Mwaipopo akiendesha baiskeli mkazi wa Vwawa ambaye ni dereva wa bodaboda.

Alisema kuwa marehemu alikuwa amempakiza mtu kwenye baiskeli na abilia wake Nione Sanga alijeruhiwa katika ajali hiyo na anapatiwa matibabu kmatika Hospitali ya Vwawa wilayani Mbozi.

Aliongeza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Vwawa na dereva wa gali hiyo alitoloma mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo.

Alisema kuwa katika ajali ya tatu, Sailosi Cheyo aligonwa na Lori aina ya Fawn a kusababisha kifo chake papo hapo wakati akijalibu kuvuka barabara.

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea katika maeneo ya kijiji cha Chimbuya Wilayani Mbozi na gali hilo lenye namba za  usajili T 509 BNP lenye tela namba T 231 BME likitokea Fingo Sijabaje mkazi wa Forest Jijini Mbeya.

Alisema kuwa ajali hiyo ilitokea mara baada ya galihiyo kuacha njia na kumvaa mtembea kwa miguu huyo na kusababisha kifo chake.
MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUFANYA USAHILI NA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI YATOL,EA KWENYE TOVUTI YA POLISI

POLISI YA TANGAZA MAJINA YA WALIOTEULIWA BOFYA HAPA

Kategori

Kategori